Wakati
2023-06-09
Maelezo
I: Sawasawa basi asante ngoja a tuchukue picha nyingine imesajiliwa kwa namba 2018_18424_2 hebu angalia unaweza ukafahamu hicho ni kitu gani?
R: Hiki ni kibao cha mbuzi
I: Kibao cha mbuzi?
R: Eeeeh
I: Kibao cha mbuzi ndiyo jina lake au kuna jina?
R: Mbuzi
I: Ni mbuzi?
R: Jina ni mbuzi
I: Haina jina la kikabila labda kisambaa mnaitaje?
R: Kwenye kisambaa tunaita tu mbuzi
I: Mbuzi?
R: Eeeh
I: Kwahiyo ni kibao cha mbuzi?
R: Mbuzi
I: Na kibao cha mbuzi kilikua kikitumika zaidi na watu wa utamaduni gani?
R: Hiki wasambaa, wabondei, wadigo watu wengi kabila nyingi za pwani pwani na wasambaa siyo sana kuliko mbondei na mdigo eeeh
I: Kwanini Zaidi wabondei na wadigo?
R: Hawa wabondei na wadigo hata zao linalotumika kwa hii mbuzi wanayo
I: Ni zao gani?
R: Minazi
I: Nazi?
R: Eeeeh inatumika tu kwa nazi
I: Kwa nazi?
R: Eeeeh
I: Kwahiyo ilikuwa inatengenezwa Zaidi mikoa ambayo nazi zinapatikana?
R: Eeeeh
I: Kama mikoa gani na mikoa gani unaweza ukaifahamu?
R: Yani mkoa wa Tanga ambapo wilaya ya kuanzia Korongwe, Muheza, Tanga na Morogoro maeneo hayo yote yanayopatikana nazi ndiyo kweli huwezi kumkosa mtu ana hii mbuzi
I: Mbuzi?
R: Eeeh
I: Na mbuzi inatumikaje sasa?
R: Hii mbuzi inatumika kwa kukunia nazi
I: Kukunia nazi?
R: Eeeh
I: Unaweza kutuambia jinsi ambavyo inafanya kazi?
R: Eeeh
I: Ehee
R: Hii inafanya kazi nazi unaichukua unaipasua ukiipasua unachukua sahani unaiweka chini ya haya meno haya unakuna sasa nazi
I: Unakuna?
R: Eeeeh
I: Baada ya hao ukishakuna?
R: Baada ya hapo ukishakuna sasa unachukua mbuzi unaikunja unaiweka pembeni unachukua nazi yako unaichuja tayari kwa matumizi
I: Nani watu gani walikuwa wakitumia zaidi mbuzi?
R: Wanawake
I: Wa umri gani?
R: Kuanzia miaka kumi kwenda juu
I: Kwanini?
R: Kwanza kuanzia hata miaka saba wengine wanawafundisha watoto miaka saba anakuna nazi kwahiyo wanafundishwa mapema tu
I: Kwanini wanawake zaidi?
R: Wanawake ndiyo wajikoni hiki hiki kinatumika sana jikoni
I: Wanawake wa jikoni hahahahahhaa
R: Eeeeh
I: Wanawake ndiyo wa jikoni?
R: Sasa wababa wanakuna nazi lakini siyo fani yao sana eeh lakini wanawake ndiyo sana wanapika
I: Sawasawa kwa mawazo yako unafikiri inaweza ikafika wakafi mbuzi haina thamani tena au haitumiki kwa makabila uliyoya taja?
R: Hii mbuzi haitaishia japo sasa hivi kuna mambo ya kisasa kuna Brenda za kusagia nazi lakini hii haitapotea kwasababu watu wote siyo wenye uwezo wa hizo Brenda eeh hii niya kiutamaduni Zaidi
I: Ya kiutamaduni zaidi?
R: Eeeeh haitapotea hii
I: Kwahiyo ikifikia wakati kila mtu anauwezo mzuri wakununua Brenda unadhani mbuzi itaendelea kutumika tena?
R: Watu wote kabisa hata wa hali za chini
I: Eeeeeh hahhhahahhha
R: Inaweza isitumike lakini itakuwa vigumu kabisa inaweza isitumike lakini ipo maana hata sasa watu wanatumia Brenda ila mbuzi zao wanazo eeh
I: Sawasawa labda ili utumie mbuzi unatakiwa uwe na kitu gani kingine?
R: Mbuzi kwenye hii kazi hapa uwe na panga la kupasulia hii nazi uwe na sahani ya kukunia hii nazi uwe na chujio la kuchujia hii nazi eeh
I: Vyote vinaenda sambamba?
R: Vyote vinaenda pamoja
I: Lazima ukitumia mbuzi hivyo viwepo
R: Ehee ndiyo
I: Sawa sawa na mbuzi bado zinatengenezwa kwa kipindi cha sasa?
R: Ndiyo zinatengenezwa
I: Kwanini unadhani zinaendelea kutengenezwa?
R: Bado matumizi yanaendelea eeh na watu wanaongezeka mwenye mbuzi leo mwingine amekua hana mbuzi kwahiyo mafundi wa mbuzi wanaendelea tu kutengeneza
I: Ni watu gani wanatengeneza mbuzi kati ya wanawake na wanaume?
R: Wanaume
I: Wanaume?
R: Eeeeh
I: Wakuanzia umri gani?
R: Kama mvulana ni mtundu hata miaka kumi na mbili anaweza akatengeneza kumi na mbili, kumi na tano na kuendelea
I: Kwanini wanawake hawatengenezi mbuzi?
R: Hizi kazi zimegawanyika kuna kazi za wanawake na kazi za wanaume kwahiyo hii imebase sana kwenye kazi za wanawake sawa sawa na kazi za uwashi mafundi wakutengeneza meza, vitanda Zaidi ni wanaume siyo kwamba mwanamke akifundishwa hawezi fanya hawezi angeweza lakini sasa kwenye mgawanyo wa kazi zipo kabisa zilizobase kwa wanaume na zipo zilizobase kwa wanawake eeh
I: Nani mikoa gani hasa wanatengeneza mbuzi?
R: Yani mkoa wa morogoro Zaidi, na huku mikoa ya watu wa wapi huku yani hizi mbuzi hata mkoa wa Tanga zinatengenezwa Morogoro, huko mbeya pia lakini kule bara pia siyo Zaidi watengenezaji sana mikoa hii ya Tanga na Morogoro
I: Sawasawa na unaweza ukafahamu ni kitu gani kilitumika kutengeneza mbuzi?
R: Miti
I: Miti na nini kingine?
R: Miti na vyuma
I: Vyuma?
R: Na kisu, panga, ya kutobolea haya matundu yakae vizuri kwa jina lingine wanaita patasi sijui
I: Patasi?
R: Eeeeh
I: Na kwasasa vifaa vinavotumika au material au nyenzo zinazotumika kutengenezea mbuzi zinabadilika au ni hizo hizo kila wakati?
R: Ndiyo hizo hizo eeh
I: Na ukiangalia mbuzi hiyo kwasasa inaweza ikauzwa shilingi ngapi?
R: Hii kwasasa hii mbuzi kama hii unaweza ukanunua kwa shilingi elfu kumi na tano
I: Elfu kumi na tano?
R: Eeeeeh
I: Pesa ya kitanzania?
R: Eeeeeeh Kumi na nne kwa kumi na tano na kuendelea
I: Hahahahahha kama ya kwenu inafanana kabisa
R: Imefanana kabisa bali ya kwangu ina meno huku na huku
chanzo: Amani-Stade Project / Amani Field Research 2023, Interview No. 03
mwandishi: I: Mohamed Seif, R: Anonymous
Mtu
-
National Institute for Medical Research (NIMR)
(Mteja)
-
unknown actor
(wissenschaftlicheR BearbeiterIn)
Mahali